Yakiwa
yamebakia masaa kadhaa kuanza kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia
2018 nchini Urusi , tayari klabu kubwa tatu kutoka Hispania
wachezaji wao watashinda kombe hilo kwa namna yoyote ile. Ivan Rakitic akikabiliana na Luka Modric kwenye moja ya mchezo wa El-Clasico. (Wote ni wachezaji wa Croatia)Klabu
ya Barcelona , Real Madrid na Atletico Madrid ndio klabu
zilizotoa wachezaji wengi kwenye mchezo wa fainali kati ya
Croatia na Ufaransa, wachezaji watatu kwa kila timu.
Wachezaji
wa Barcelona watakaotumikia leo timu zao za taifa ni Samuel Umtiti ,
Ousmane Dembele wote Ufaransa na Ivan Rakitic wa Croatia. Samuel Umtiti , Ousmane DembeleWachezaji kutoka Real Madrid ni Luka Modric na Mateo Kovačić wote wa Croatia huku Raphael Varane akiitumikia Ufaransa. Luka Modric na Mateo KovačićKwa
upande wa Atletico Madrid , wachezaji watakaoiwakilisha klabu hiyo
kwenye mchezo wa fainali ni Sime Vrsaljko kutoka Croatia na Lucas
Hernandez na Antoine Griezmann wote wa Ufaransa. Lucas Hernandez na Antoine GriezmannKatika maana nyingine ni kwamba klabu hizo kwa matokeo yoyote yale ni lazima wachezaji wao wachukue kombe la Dunia leo.
0 comments:
Post a Comment