HATIMAYE
klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam imetangaza rasmi kuwarejesha viungo
wake, Deus Kaseke na Mrisho Ngassa ili kuimarisha kikosi chake kuelekea
mechi zilizosalia za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika.
Sasa
mashabiki wa Yanga wanasubiri kusikia mshambuliaji Heritier Makambo
kutoka DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambaye
inaelezwa jina lakde limetumwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) pamoja
na Ngassa na Tegete kwa ya kucheza Kombe la Shirikisho.
Ngassa
na Kaseke wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa rasmi Yanga
kufika wanne, baada ya viungo wengine, Feisal Salum kutoka JKU ya
Zanzibar na Jaffar Mohammed kutoka Maji Maji ya Songea iliyoshuka
Daraja.
Mrisho
Ngassa (kushoto) aktia dole gumba katika fomu za mkataba wa Yanga
pembeni ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika
Lakini uongozi wa Yanga unakabiliwa na mtihani juu ya wachezaji waliogoma, kipa Benno Kakolanya, mabeki Juma Abdul, Andrew Vincent ‘Dante’, Hassan Kessy na Kelvin Yondan ambao wamemaliza mikataba wanataka wasaini mipya.
Lakini uongozi wa Yanga unakabiliwa na mtihani juu ya wachezaji waliogoma, kipa Benno Kakolanya, mabeki Juma Abdul, Andrew Vincent ‘Dante’, Hassan Kessy na Kelvin Yondan ambao wamemaliza mikataba wanataka wasaini mipya.
Wachezaji
wote hao wamesusa mazoezi wakishinikiza kupewa mikataba mipya na
angalau Kakolanya, Abdul na Dante walifanya mazoezi kwa siku kadhaa
kabla ya leo kuungana na Kessy na Yondan kususa kabisa kufuatia kuona
viongozi hawatimizi ahadi.
Yanga
SC inatarajiwa kuteremka uwanjani Jumatano ya Julai 18, mwaka huu mjini
Nairobi nchini Kenya kumenyana na wenyeji, Gor Mahia nchini Kenya
katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika, kabla ya timu hizo
kurudi Dar es Salaam kwa mchezo wa marudiano Julai 29.
Yanga
SC haijashinda mechi hata moja kati ya mbili za awali za Kundi D Kombe
la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa 4-0 na USM Alger nchini Algeria
Mei 6 na kutoa sare ya 0-0 na Rayon Sports ya Rwanda mjini Dar es Salaam
Mei 16.
Baada
ya hapo, Yanga SC itacheza tena nyumbani, Uwanja wa Taifa
ikiwakaribisha USM Alger Agosti 19 kabla ya kwenda kukamilisha mechi
zake za kundi hilo kwa kumenyana na wenyeji, Rayon Sport Agosti 28.
Timu
mbili za juu katika kundi hilo zitaungana na washindi sita wa makundi
mengine manne kwa mechi za nyumbani na ugenini za Robo Fainali na
zitakazofuzu zitasonga mbele, Nusu Fainali na baadaye Fainali.
Bingwa
wa Kombe la Shirikisho atapata zawadi ya dola za Kimarekani, 1 250,
000, mshindi wa pili dola 432, 000 wakati timu zitakazoshika nafasi za
pili kwenye kila kundi zitapata dola 239, 000 kila moja, nafasio ya tatu
dola 239, 000 na za nne dola 150, 000.



0 comments:
Post a Comment