Mdau
na mwanasoka wa zamani hapa nchini, Kenny Mwaisabula maarufu kama
Mzazi, amefunguka kwa kusema kuwa wachezaji wengi wa kigeni wanafeli
kutokana na kuendekeza starehe.
Mwaisabula
ameeleza wachezaji wengi kutoka nje ya nchi wamekuwa wakifika nchini
wakiwa na viwango vizuri lakini baada ya muda wanapotea kwenye ramani.
Mdau
huyo amemtaja mchezaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, kuwa ni moja
ya wachezaji ambao kwa sasa hawana makali kama alivyotua wakati anatokea
Power Dynamos ya Zambia.
Ameeleza
kuwa starehe imemgharimu Chama na sasa hana tena ule umaridadi ndani ya
dimba kitu ambacho kimesababisha kiwango chake kuporomoka.
"Chama
ninayemfahamu mimi si yule wa Simba aliyekuwa mzuri kwa mwaka jana,
wachezaji wengi wa nje wakija Tanzania hawamalizi mwaka mmoja wanapotea
dimbani, starehe wanaendekeza zaidi kuliko kazi",

0 comments:
Post a Comment