
Winga wa Borussia
Dortmund Jadon Sancho, anataka kuondoka katika ligi kuu ya Ujerumani,
huku viongozi wa ligi ya Premia Liverpool wakiwa miongoni mwa vilabu
vinavyomtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa England wa miaka 19. (Mail)
Beki
wa kushoto na mlinzi wa safu ya nyuma wa England na Tottenham Hotspur
Danny Rose, 29, ameapa kukatiza miezi 18 ya mwisho ya mkataba wake baada
ya kuambiwa kuwa hatapewa mkataba mpya. (London Evening Standard)Spurs inahofia kuwa kiungo wa kati wa Denmark wa miaka 27- Christian Eriksen, Jan Vertonghen, 32 na beki Mbelgiji mwenzake Toby Alderweireld, 30, watafuata hatua sawa na ya Rose na kuondoka kwa uhamisho wa bure mikataba yao itakapokamilika msimu ujao . (Star)

Meneja wa Uholanzi Ronald Koeman amesema kuna uwezekano wa yeye kupata kazi Barcelona baada ya michuano ya Euro 2020. (Marca)
Winga wa Chelsea na Brazil Willian, ambaye mkataba wake Stamford Bridge unamaizika msimu ujao, analengwa na Juventus na Barcelona, na huenda wakajaribu kumsaini kiungo huyo wa miaka 31 mwezi Januari wakiafikiana . (Mirror)

Mchezaji wa Manchester City David Silva, 33, anaelekea kujiunga na Mhispania mwezake wa miaka 35 anayecheza safu ya kati Andres Iniesta katika klabu ya Japani ya Vissel Kobe mkataba wake katika uga wa Etihad utakapokamiliki msimu ujao. (Mail)

Napoli huenda ikalazimika kumuuza mlinzi wa Senegal wa miaka 28 Kalidou Koulibaly, amabye amehusishwa na uhamisho wa Manchester United, huku mshambuliaji wa Ubelgiji wa miaka 32 Dries Mertens, akinyatiwa na Arsenal. (Ilmattino - in Italian)

Mkurugenzi wa michezo wa Juventus Fabio Paratici ameonekana Manchester, huku tetesi zikiashiria kuwa anafuatilia mpango wa kubadilishana wachezaji utakaomhusisha kiungo wa kati wa Manchester United wa miaka 26- Mfaransa Paul Pogba na mashambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic, 33. (talksport)

0 comments:
Post a Comment