Monday, November 4, 2019


Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa kinda wa Arsenal, Gabriel Martinell ndiye mchezaji bora kijana wa sasa.

Kinda huyo aliwasha moto kwenye mchezo wa Kombe la Carabao hatua ya 16 bora dhidi ya Liverpool.

Kinda huyo alitupia mabao mawili kwenye mchezo huo ambao Arsenal walifungwa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya mabao 5-5.

 "Martinell kwangu ndiye mchezaji bora kijana kwa sasa duniani, ana kiwango cha hali ya juu sana na anajua kufunga mabao," amesema.

0 comments:

Post a Comment