OLE
Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa
hamtambui mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Robin
Van Persie ambaye alimchana kwa kitendo chake cha kuonyesha tabasamu
licha ya kufungwa na Arsenal.
United
ilichapwa mabao 2-0 na Arsenal kwenye mechi ya Ligi Kuu England
iliyochezwa Jumatano, Uwanja wa Emirates ila Solskkjaer alionekana
kutabasamu wakati wa mahojiano na waandishi wa habari jambo ambalo Van
Persie aliponda suala hilo.
Van
Persie alitoa maoni yake kwenye kipindi cha BT Sport baada ya kuona
mahojiano ya Solkjaaer uwanja wa Emirates Jumatano usiku.
"Simjui
Robin na Robin hanijui mimi, hana mamlaka na nguvu ya kunikebehi kwa
namna anavyofikiria hiyo sio sawa namna yangu ya utawala na misimamo
yangu haiwezi kubadilika," amesema.
0 comments:
Post a Comment