HARUNA
Niyonzima, kiungo wa Yanga mwenye ufundi wake uwanjani, tayari
ameshakabidhiwa viatu maalum tayari kwa kuhakikisha anawagaragaza
walinzi na viungo wa Simba leo Jumamosi.
Simba
anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Yanga leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, ni mara ya kwanza timu hizi
zinakutana msimu huu, mchezo wao wa mwisho Simba ilishinda bao 1-0.
Niyonzima
ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo
la usajili ambalo lipo wazi tangu Desemba 16, mwaka jana na utafungwa
Januari 15, mwaka huu.
Niyonzima
alitua nchini juzi Alhamisi akitokea kwao Rwanda na Ofisa Habari wa
Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kiungo huyo amekabidhiwa vifaa vyake
ikiwemo viatu maalumu tayari kwa kuwamaliza Simba leo.
“Niyonzima
tayari ameshakabidhiwa viatu vyake kwa ajili ya mchezo wa kesho (leo)
pamoja na jezi ikiwa ni utaratibu wa klabu hata kama mchezaji amekuja na
vifaa vyake, hivyo ni lazima apewe vifaa vipya, hata wachezaji wengine
wapya wamepewa baada ya kutua,” alisema Bumbuli.
0 comments:
Post a Comment