KOCHA Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard amesema kuwa mpango wake mkubwa msimu huu ni kuwauza nyota wake nane ndani ya kikosi hicho.
Lampard
ambaye aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Chelsea na alifundishwa na
Jose Mourinho ambaye ni Kocha Mkuu wa Spurs inayoshiriki Ligi Kuu
England ila walipokutana naye msimu huu kwenye mechi zao za ligi
alimpiga nje ndani mwalimu wake.
Miongoni
mwa wachezaji ambao amepanga kuwauza ni pamoja na Kepa
Arrizabalaga,Ross Barkley na Jorginho hawa wapo kwenye hesabu za kuuzwa
msimu huu.
Marcos
Alonso, Emerson, Kurt Zouma, Willian na Pedro ni miongoni mwa nyota hao
anaotarajia kuwauza kutokana na kile anachoeleza kuwa wameshindwa
kutimiza majukumu yao kwa ukamilifu.

0 comments:
Post a Comment