
Kocha wa timu ya taifa ya soka
nchini Kenya, Stanley Okumbi amewaita wachezaji 26 kambini kwa minajili
ya mechi ya kirafiki dhidi ya Angola tarehe 4 mwezi ujao.
Mchuano
huo wa kimataifa utapepetwa mjini Machakos mashariki mwa taifa hilo
huku mechi hiyo ikitumika kuiandaa Kenya kabla ya kombe la CHAN mwaka
ujao. Hata hivyo kikosi hicho kimewajumuisha wachezaji wanaocheza soka ya kulipwa nyumbani pekee. Wataripoti kambini mapema wiki ijayo kwa maandalizi zaidi.
0 comments:
Post a Comment