
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameikabidhi bendera timu ya Azania
ambayo inaelekea nchini Uingereza kushiriki mashindano ya Standard
Chartered Safari kwenda Anfield.
Akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi bendera pamoja na hati za kusafiria, Waziri Mwakyembe alisema
ni fursa ya kipekee ambayo Tanzania imeipata kushiriki mashindano kama
hayo na ni muda sasa dunia kujua kuwa Tanzania kuna vipaji vya soka
hivyo wahakikishe wanarudi nchini na kikombe."Mtuwakilishe vyema huko muendako ni muda sasa wa dunia kuwa Tanzania tuna uwezo wa kisoka, kila mmoja acheze vizuri na kuonyesha uwezo wake, tunaamini mtarudi na kikombe na nawatakia kila la kheri," alisema Waziri Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera pamoja na hati za kusafiria kwa timu ya Azania ambayo inaelekea nchini Uingereza kushiriki mashindano ya Standard Chartered Safari kwenda Anfield iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar Es Salaam.
Nae Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered Tanzania, Ami Mpungwe amesema benki yao inajivunia kupata wawaklishi kutoka Tanzania na wamesimamia gharama zote za safari kwa muda wote ambao timu itakuwa Uingereza na ni matumaini yao kuwa timu hiyo ya Azania itarejea nchini na kikombe.
"Tupo hapa kuiaga timu ya Azania ambao ni mabingwa wa Tanzania na Afrika Mashariki wa kombe la Standard Chartered Safari kwenda Anfield, tunajivunia timu hii sababu imetuletea heshima kubwa, tunawaombe ushindi mkubwa na tunategemea watakuja na ubingwa," alisema Mpungwe.
Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke akitoa pongezi kwa timu ya Azania kupata nafasi ya kwenda Uingereza wakati wa hafla ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo inayokwea pipa kesho 18 Mei. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
0 comments:
Post a Comment