Wednesday, May 17, 2017



 Baadhi ya wasimamizi wa kamati ya Olimpiki
 walioketi ni Wasimamizi wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya.



Wasimamizi wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya, NOCK, wameshtakiwa kwa njama za wizi na usimamizi mbaya wa fedha na sare za kikosi cha Kenya katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika mjini Rio , Brazil mwaka uliopita.
Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya, ODPP imetangaza kuwa, baada ya kutathmini uchunguzi, maafisa hao wanastahili kushtakiwa kwa makosa hayo.
Wasimamizi hao wakiwemo msimamizi wa timu ya Kenya kwenye Olimpiki, Stephen Soi, aliyekuwa naibu mkuu wa ujumbe wa Olimpiki, Bernard Ekumbo, katibu mkuu, FK Paul na naibu meneja wa timu hiyo, Pius Ochieng watafikishwa mahakamani baadaye mwezi huu kujua hatma yao

0 comments:

Post a Comment