Roger Federer: Sitoshiriki mashindano ya wazi ya Ufaransa ‘ French Open’
|
Mcheza Tenisi anaeshika nafasi ya 5 katika viwango vya ubora Ulimwenguni na mshindi wa mashindano ya wazi ya Ufarasa ya mwaka 2009, Roger Federer , ametangaza hatoshiriki mashindano ya safari hii ya wazi ya Ufaransa {French Open}.
Mcheza Tenisi raia wa Uswisi,Roger Federer
Roger Federer, ametangaza kutoshiriki ili apate muda wa kujiimarisha pamoja kufanya maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Wimbledon. Legendari huyo raia wa Uswiss ambaye hakushiriki mashindano ya 18 ya wazi ya Australia ya mwezi Januari baada ya kutokuwa katika mchezo huo kwa miezi 6 kutokana na kupata majeraha Mei 28 mwaka jana.
Mcheza Tenisi raia wa Uswisi,Roger Federer
Federer,aliweka barua katika tovuti yake siku ya Jumatatu ikielezea kutoshiriki na anajiskia vibaya kwake kukosa kushiriki katika michuano hiyo mikubwa, “Kwa bahati mbaya sitoshiriki mashindano ya wazi ya Ufaransa”
0 comments:
Post a Comment