Tayari aliyekuwa golikipa wa Man City Willy Caballero ameshakamilisha usajili kwenda Chelsea na kinda Ethan Ampadu naye tayari ameshamwaga wino kuitumikia klabu hiyo.
Bado Antonio Conte anapambana kununua wachezaji ili kuzidi kukiimarisha kikosi chake na hatimaye hata kutetea taji lao walilonalo la Premier League katika msimu ujao wa ligi ya Uingereza.
Ripoti zinasema klabu hiyo ya Chelsea na klabu ya As Roma zimeshafikia makubaliano kwa ajili ya kumnunua beki wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ujerumani Antonio Rudiger ambaye wamekuwa wakimtafuta siku nyingi.
Wakati Rudiger akikaribia kusaini katika klabu hiyo ya Chelsea, mlinzi mwingine toka Juventus Alex Sandro naye yuko njiani ndani ya siku chache sisizozidi saba kumwaga wino wa kuichezea Chelsea.
Wakati walinzi hao wakijiunga Chelsea kuna kiungo toka Monaco Timoue Bakayoko naye taarifa zinasema uhamisho wake kwenda katika klabu ya Chelsea umekaribia na siku chache zijazo anajiunga nao.
Pamoja na manunuzi yote haya lakini mashabiki wa Chelsea bado hawana raha kwani hadi sasa hakuna dalili ya klabu hiyo kumnunua mshambuliaji mkubwa kwani Lukaku,Rodriguez na Morata wote wamekuwa wagumu kununulika.
0 comments:
Post a Comment