- Details
- Created: Monday, 03 July 2017 20:50
SOMA ZILIZOBAMBA ENGLAND:
BABA, WAKALA WA MORATA
WAWAKILISHI wa Straika wa Spain Alvaro Morata wamekutana na Real Madrid Asubuhi hii kujadili hatima ya Straika huyo anaetaka kwenda Manchester United.
Manchester United wanataka kumsaini Morata ili ambadili Zlatan Ibrahimovic huku akiafiki Uhamisho huo.
Hii Leo, Wakala wa Morata, Juanma Lopez, na Baba Mzazi wa Mchezaji huyo, Alfonso Morata, walitua huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid na kufanya Mazungumzo ya Dakika 50 na Real Madrid.
Man United na Real zimekuwa zikivutana kuhusu Dau la Uhamisho ambalo Real wanataka Zaidi Pauni Milioni 70 kwa Straika huyo wa Miaka 24 wakati Man United walishatoa Ofa ya Pauni Milioni 52.4.
Everton yamsaini Straika wa Malaga Sandro Ramirez
Straika wa Malaga, Sandro Ramirez, amesaini Mkataba wa Miaka Minne na Everton.
Msimu uliopita Chipukizi huyo wa Miaka 21 alifungia Malaga Bao 14 baada ya kujiunga nao kutoka Barcelona.
Everton wanatarajiwa kumasaini Beki wae, kwa Dau la Pauni Milioni 24.
Tayari Everton wameshawasaini Kipa wa England U-21 kutoka Sunderland,Jordan Pickford, kwa Pauni Milioni 30 na Kepteni wa Ajax ya Netherlands, Davy Klaasen, kwa Pauni Milioni 24.
Aston Villa yamsaini Kepteni wa zamani wa Chelsea na England John Terry
John Terry, mwenye Miaka 36, amesaini kuichezea Aston Villa ambayo sasa inacheza Daraja la chini yake EPL, LIGI KUU ENGLAND.
Terry, ambae Mkataba wake na Chelsea uliisha Juni 30, amedai alikataa kuchezea Klabu za EPL kwa vile hataki kuikabili Chelsea.
Akiwa na Chelsea, Terry aliichezea Mechi 717 na kutwaa Ubingwa wa EPL mara 5
0 comments:
Post a Comment