Michuano ya mchezo wa Tennis ya Wimblendon imeanza hii leo kwa mchezo kati ya bingwa mtetezi wa michuano Andy Murray aliyekuwa uwanjani dhidi ya Alexandre Bulbik.
Kabla ya mchezo huo hofu ilitada kwa mashabiki wa Murray kwani siku chache tu kabla ya michuano hii kuanza kulikuwa na hofua kuhusu Murray kushiriki kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo.
Lakini hata hivyo Murray akicheza mbele ya mke wake mjamzito Kim amefanikiwa kuibuka kidedea kwa kushinda seti zote dhidi ya Bulbik, Muingereza huyo alishinda mchezo wa leo kwa seti 6-1 6-4 na 6-2.
Alexandre Bulbik raia wa Khazakhstan alipewa nafasi na wengi wakiamini anaweza kuishangaza dunia dhidi ya Murray ambaye alionekana hayuko fiti.
Baada ya ushindi huo sasa Murray anakwenda kukutana na Dustin Brown raia wa Ujerumani katika raundi ya pili na ikumbukwe Brown alishawahi kumfunga Rafael Nadal katika michuano hii mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment