SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifutia adhabu ya kuifungia Sudan baada ya Serikali ya nchi hiyo kujisafisha.
Mapema mwezi huu nchi hiyo ilifungiwa na FIFA baada ya Serikali yake kuingilia shughuli za soka.
hata hivyo, Serikali ya Sudan ikabadilisha maamuzi iliyofanya hadi kuiponza Sudan kufungiwa FIFA.
"Kwa hali hiyo, (FIFA) imeamua kuondoa adhabu ya kuisimamisha (Sudan) mara moja,"imesema barua ya Katibu wa FIFA, Mama Fatma Samoura.
Kuondolewa kwa adhabu hiyo kunakuja wakati tayari Sudan imeathirika baada ya klabu zake kubwa, El Merreikh na El Hilal kuondolewa kwenye michuano ya Afrika kutokana na kufungiwa na FIFA.
Katibu wa FIFA, Mama Fatma Samoura amewaandikia barua Sudan kuwaarifu kufutiwa adhabu
El Merreikh ilikuwa kwenye nafasi ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa wakati El Hilal Obeid ilitolewa kwenye Kombe la Shirikisho ikiwa tayari imetinga Nane Bora.
Pamoja na hayo, taifa hilo sasa litaendelea na mechi za kufuzu Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2018 Kenya inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee kwa kucheza mechi ya kwanza na Burundi.
Sudan ilifungiwa baada ya Waziri wa Sheria kumuondoa madarakani Rais wa Chama cha Soka (SFA), Mutasim Gaafar Sir Elkhatim Juni 2, mwaka huu kufuatia mgogoro uliotokea ndani ya chama hicho na kuugawa uongozi wake makundi mawili.
Hatua ya FIFA inakuja baada ya Waziri Mkuu wa Sudan, Bakri Hassan Salih kubadilisha maamuzi hayo Julai 7 na kumrudisha madarakani Elkhatim.
Klabu za Sudan zilitarajiwa kucheza kati ya Julai 7 na 9 kwenye michuano ya Afrika, lakini barua ya FIFA ikawaondoa mashindanoni.

0 comments:
Post a Comment