Achana na habari ya Wladmir Klistchko kustaafu ndondi lakini
gumzo kubwa katika wikiendi hii katika ulimwengu wa masumbwi ni bondia
Amir Khan, mkewe Fryal Makhdoom na bondia mwingine wa Uingereza Anthony
Joshua.
Amir Khan amemtuhumu Anthony Joshua kwamba anatembea na Makhdoom,
huku Khan akisema kwamba Joshua ndio chanzo cha yeye na mkewe huyo
kutalakiana suala ambalo Anthony Joshua amesema sio kweli hata kidogo.
Mtafaruku huu ullianzia katika ukurasa wa Twitter wa Khan baada ya
Khan kutupa kijembe kwa Anthony na Makhdoom kuwa wawili hao ni wapenzi
na kusisitiza hilo hata halimuumizi kichwa hata kidogo.
Amir Khan aliandika mambo mengi huku moja ya tweet akiandika
“mwanamke wangu aliniambia anataka kuwa na mwanaume mwingine ambaye ni
Anthony Joshua” na baadae akaandika “hata sina wivu na sihitaji kutumiwa
picha za mwanaume mwingine”
Khan alienda mbali zaidi na kutuma screen shot ya mawasiliano kati ya
mkewe na mtu aliuyesomeka kwa jina la Ghost wakipanga kuonana huku
Ghost mwenyewe akidhaniwa ni Joshua lakini baadae Khan alisema yeye na
mkewe wameamua kutengana.
Baadaye mke wa Khan aliibuka naye mtandaoni akimshambulia mumewe kwa
kusema kwamba “hakukuwa na haja ya kupost tweet za kijinga vile” huku
akidai Khan amekwisha kimasumbwi na hivyo anataka watu wamkumbuke ndio
maana akafanya hivyo.
Baada ya mke wa Khan kusema account ya Khan ilihakiwa, mshambuliaji
huyo aliibuka tena kupitia mtandao wa Snap Chat na kusema kupitia video
kwamba maneno yote aliyosema kuhusiana na mke wake yalikuwa ni ya kweli.
Kwa upande wa Anthony Joshua naye aliibuka kupitia mtandao wa Twitter
na kukanusha madai ya Amir Khan akisema “sio mimi”. Taarifa toka mjini
Dubai zinasema Fryal Makhdoom amekuwa akijaribu sana kurudisha mahusiano
yake na Khan lakini Khan amesema hawezi rudiana na Makhdoom.
Wakati Khan na Makhdoom wakiwa katika mvutano huo kumeibuka model
mwingine nchini Ufaransa aitwaye Flore Aguilar ambaye alishawahi kuwa
mpenzi wa Mario Balotelli na Ashley Cole ameibuka na kusema alishawahi
kulala na Khan wakati akiwa kwenye ndoa.
Amir Khan tayari yuko njiani kuelekea nchini Marekani baada ya kuisha
kwa wikiendi iliyokuwa ndefu kwake na sasa amesisitiza kwamba akili
yake yote anaielekeza kwenye kipaji chake na mazoezi.
Home
»
»Unlabelled
» Amir Khan amshambulia mkewe na kumshutumu kutoka na bondia mwenzake, story kamili hii hapa
Monday, August 7, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment