Monday, August 7, 2017


Arsenal hii leo wameendeleza rekodi yao ya ubabe kwa Chelsea katika mechi za fainali baada ya kuwafunga Chelsea katika hatua ya matuta hii leo katika mchezo wa ngao ya hisani.
Walikuwa Chelsea waliotangulia kwa goli la Victor Moses dakika 46 alipowafungia bao la kwanza  na kuwafanya Chelsea kuonekana kama wanaweza kumaliza dakika 90.
Ilipofika dakika ya 80 Pedro Rodriguez alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya kiungo Mohamed El Neny, na dakika mbili baadae Arsenal walisawazisha kupitia Saed Kolasanic.
Baada ya dakika 90 kuisha bila mshindi mchezo ulienda katika hatua ya matuta huku Garry Cahil alianza kuifungia Chelsea kabla ya Theo Walcott na Bellerin kuifungia Arsenal.
Baadae kipa wa Chelsea Thibaut Courtouis na Alvaro Morata nao walikosa penati, kisha mwisho wauaji wawili wa Arsenal Oxlade Chamberlain waliimaliza Chelsea.
Hii ni ngao ya hisani ya 15 kwa klabu ya Arsenal na ikiwa ni ya 3 katika misimu minne iliyopita ya vijana hao wa Arsene Wenger.

0 comments:

Post a Comment