MSHAMBULIAJI Alexis Sanchez ataukosa mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu ya England kutokana na maumivu ya tumbo.
Akiwa
amechelewa kujiunga na wenzake kwa maandalizi ya msimu mpya kutokana na
kuwa na timu yake ya taifa, Chile kwenye michuano ya Kombe la FIFA la
Mabara, Sanchez hataweza kucheza mechi dhidi ya Leicester City Ijumaa.
Lakini
Arsene Wenger amesema mchezaji wake huyo nyota yuko nje kutokana na
maumivu. "Ana maumivu madogo tumboni aliyoyapata kwenye mazoezi ya
Jumapili asubuhi kabla hajaja Wembley,".
Alexis Sanchez ameumia tumbo na atakosekana kwenye mechi za mwanzoni za msimu mpya wa Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Alifanyiwa
vipimo siku mbili zilizopita na atakuwa nje kwa muda fulani - sifahamu;
wiki mbili au wiki moja zaidi? Lakini hatakuwepo. Nafikiri
hatacheza Stoke. Kwetu, Alexis Sanchez ni pigo" alisema Wenger.
Alipoulizwa
kama Sanchez, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake atasaini
mkataba mpya, Wenger alisema: "Wakati wote inawezekana. Mchezaji
anapokuwa katika mwaka wa mwisho (wa mkataba wake) wakati wote
tutajaribu kumuongezea," alisema. "Hakuna sababu ya kutofanya hivyo.
hatujafika huko bado,"alisema.
0 comments:
Post a Comment