–
Na Mwandishiwetu , Dar es Salaam
Mgombea
Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela
ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama
atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa kampeni yake Mwakalebela
amesema kuwa kwa kuanza ataanza na Utawala bora kwa Kuweka misingi ya
wazi katika mapato na matumizi ya TFF,Kuzifanya kamati za TFF kuwa huru
na kufanya kazi bila kuingiliwa,uingalia upya Agenda ya kupunguza idadi
ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ili tuweze kupanua wigo wa wadau wa
mpira wa miguu kutuwakilisha kwa wingi katika mkutano mkuu.
amesema
kuwa pia ataweza kusimamia matakwa ya katiba ya shirikisho la mpira wa
miguu Tanzania kwa kufanya vikao na mikutano inayotambuliwa kikatiba,
kuwa na vyombo imara vya usimamizi ndani ya shirikisho ili kuleta
matokeo chanya yenye ufanisi katika soka.
Mwakalebela amesema ataweza kusaidia Timu za Taifa ,wanaume,Wanawake na Vijana kwa
Kuwa na makocha wenye viwango vya juu ikiwa ni pamoja na Kurudisha
hamasa kwa watanzania kuzipenda timu za Taifa kwa kuongeza idadi
kubwa za wachezaji wa ndani kucheza nje ya nchini pamoja na kucheza FIFA
date zote na Kuziweka timu kambini kwa wakati
aidha
katika mpango huu wa pili ataweza Kuanzisha na kusimamia Academy
nyingi Tanzania kwa kuhakikisha timu zinapata mechi nyingi za kirafiki
na kimataifa kuandaa mashindano ya kimataifa Kuwa na mfadhili wa
kugharimia mpango kazi wa timu za Taifa.
Katika mpango wake wa tatu Mwakalebela amesema atashirikiana naVilabu kwa Kupitia upya
mikataba ya sasa ili kuiboresha na kuleta tija katika vilabu pia
ameadhimia kuongeza idadi ya mashindano ili kuongeza ufanisi kwa
wachezaji na Taifa kwa ujumla.
Ameongeza
ataweza kuboresha kanuni zetu kuwa zenye tija na ufanisi hili kuongeza
mapato ya vilabu kwa kuifanya Bodi ya Ligi kuwa huru nakuweza kuboresha
viwanja vya mashindano pamoja na kuongeza idadi ya wadhamini kwa
kufanya mpira kuwa starehe na biashara.
Katika kusaidia Vyama vya Soka vya Mikoa Mwakalebela amesema kuwa
atafanikisha kupatikana kwa vitendea kazi kama
mipira,kompyuta,printers na thamani za ofisini na kuwawezesha kuwapatia
Wadhamini wa kudumu kwa ajili ya ofisi kujiendesha na kuwapatia ruzuki
za kila mwezi kwa shughuli za chama kwa kuongeza idadi ya mashindano
mikoaniKuboresha viwanja na ofisi za mikoani kuwapatia viongozi mafunzo
ya kuwajengea uwezo ndani na nje ya nchi.
Katika
kusaidia Vyama Shiriki Waamuzi,Tiba Michezo,Waamuzi,Tiba
Michezo,Makocha,Wanawake,Sputanza kwa Kutoa Mafunzo ya ndani na nje ya
nchi ili kuwajengea uwezo, Kuwapatia ruzuku kwa ajili ya shughuli za
kila siku na kuwapatia wadhamini kwa kuwapatia vitendea kazi.
Katika
kuboresha Sekretarieti Mwakalebela amesema atawezesha Sekretarieti kuwa
na watendaji wenye weledi na uwezo katika maeneo yao ya kazi kwa
Kuajiri watendaji kwa kuzingatia sifa na vigezo katika nafasi husika.
Kuongeza uadilifu katika utendaji kazi.
Kusimamia watendaji waweze kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia uhitaji wa wadau wa soka nchini.
Kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo ndani na nje ya nchi.
Katika Mahusiano na Wadau Mwakalebela amesema
Ili
kupata mafanikio chanya katika maendeleo ya soka ni lazima kuhakikisha
wadau wanashirikishwa ipasavyo, hivyo nitahakikisha natambua nafasi ya
wadau na kushirikiana nao,Serikali pamoja na Vyombo vyake,Wachezaji wa
sasa na wale wa zamani,Wanahabari, Taasisi, Mashirika na Kampuni
mbalimbali,Mashabiki na wapenzi wa mpira,Wadhamini na
wafadhili,Wamiliki wa viwanja vya michezo, Watanzania wote kwa ujumla.
Katika
uwekezaji wa Kitega Uchumi Mwakalebela ametaja kuwa Mafanikio ya mpira
yanahitaji rasilimali fedha, kwa kulitambua hilo, nitahakikisha
kunafanyika uwekezaji wa jengo la kisasa la kitega uchumi katika uwanja
wa kumbukumbu ya Karume ili kuweza kusaidia ufanikishaji .
Amesema
Uwezeshaji wa ruzuku kwa wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania,Kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu katika ngazi mbalimbali
kutokana na uhitaji,Mafunzo kwa wanachama,Vitendea kazi kwa
wanachama,Uboreshaji wa ofisi za TFF kuwa zakisasa zaidi.
Katika
kuboresha Bodi ya ligi Mwakalebela amesema Bodi ya Ligi itakuwa huru
kwa kuijengea uwezo kwa kuongeza wafadhili na Kuwa na Mpango kazi ambao
utasaidia kuifanya bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi pasipo
kuingiliwa.
Katika
kuboresha Miundombinu Mwakalebela amesema kuwa kwa Kushirikiana na
wamiliki wa viwanja ataweza kuviboresha hili kuwa na nyasi bandia
katika kila kanda kwa kuwa na Viwanja vyenye hadhi na sio kuta tu peke
yake.
0 comments:
Post a Comment