BEKI Dani Carvajal amesaini mkataba mpya na Real Madrid ambao
ndani yake una bei ya kumuuza ambayo si rahisi mchezaji mwenyewe
amesema; "Ni bei kubwa sana, hivyo kwamba hakuna yeyote anayeweza
kunitoa hapa,".
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye ameichezea Real Madrid mechi 167,
amesaini mkataba mpya leo ambao utamuweka pamoja na klabu hiyo ya La
Liga hadi mwaka 2022.
Kufuatia
kuondoka kwa Neymar kwa dau la Pauni Milioni 198 kwenda Paris
Saint-Germain msimu huu, mkataba wa Carvajal unahusisha na kipengele cha
kuuzwa kwa Pauni Milioni 308 - bei ambayo beki huyo anatumai
itamuhakikishia kudumu hadi mwisho wa mkataba wake katika klabu hiyo.
Dani Carvajal akipewa jezi namba 2022 kuashiria kusaini mkataba ambao utamalkizika mwaka 2022 Real Madrid PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Klabu
hii ni sehemu kubwa ya maisha yangu, hivyo kwangu huku ni kukamilika
kwa ndoto zangu,"amesema baada ya kuongeza muda wake wa kuendelea
kufanya kazi Bernabeu.
Carvajal aliibukia katika akademi ya vijana ya Real Madrid kabla ya kuhamia Bayer Leverkusen ya Ujerumani mwaka 2012.
Alirejea katika klabu yake ya utotoni mwaka mmoja baadaye na tangu hapo amekuwa mmoja wa mabeki bora wa kulia duniani.
Na amesema anafikiria simu moja kurithi kitambaa cha Unahodha wa klabu kutoka kwa Nahodha wa sasa, Sergio Ramos.
0 comments:
Post a Comment