
Rio Ferdinand anazindua taaluma yake mpya kama mwanandondi miaka miwili baada ya kustaafu kutoka soka.
Hatua
ya Rio mwenye umri miaka 38 kujiunga na ndondi imeiungwa mkono na
kampuni ya kamari ya Betfair ambayo ilitangaza taraifa hizo leo Jumanne.Mlinzi huyo wa zamani wa England na Manchester United pia ana kampuni yake ya nguo.
"Ninafanya hivi kwa sababu ni changamoto," alisema Rio." Nimeshinda mataji na sasa ninalenga kushinda mkanda."
Aliyekuwa nahodha ya kikosi cha kriketi cha England Andrew Flintoff, pia naye alizindua taalumaa ya ndondi baada ya kustaafu, alipata ushindi mwaka 2012 dhidi ya Mmarekani Richard Dawson kwa pointi.
Ni kampuni ya Betfair iliyomuomba Ferdinand kuanzisha taaluma hiyo na itamsaidia kufuzu na kupata leseni ya bodi ya ndondi ya Uingereza kabla ya kuanza kujifunza na kushindana
0 comments:
Post a Comment