Thursday, September 7, 2017

Ghanaian referee Joseph Lamptey

Mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya Afrika Kusini na Senegal itarudiwa tena baada ya refa aliyesimamiwa mechi hiyo kupigwa marufuku na Fifa.
Refa huyo raia wa Ghana Joseph Lamptey, alipiwa marufuku kwa kusimia mechi kwa njia isiyofaa.
Aliwapa penalti Afrika Kusini ambao walishinda kwa mabao 2-1 mwezi Novemba mwaka uliopita kwa kunawa mpira lakini kanda ya video baaadaye ilionyeha kuwa mpira huo ulimgonga kwenye goti mlinzi wa Senegal Kalidou Koulibaly.
Mechi hiyo itachezwa tena Novemba mwaka huu.
Lamptey alipigwa marufuku ya maisha mwezi Machi lakini jana Jumatano marufuku hiyo ilibatiliswa na mahakama ya michezo. 
a Fifa headquarters
Lamptey, ambaye pia alisimamia mechi katika mashindano ya Olimpki huko Rio mwaka uliopita alikataa na kungea na BBC baada ya kupigwa marufuku ambayo ilikuja baada ya Senegal kulalamika.
Senegal na Afrika Kusini kwa saa wako nafasi ya tatu na nne mtawalia katika kundi la la D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde.
Ni timu moja pekee ya kwanza katika kundi ambayo itafuzua kwa meche za kombe la dunia nchini Urusi mwaka ujao.

0 comments:

Post a Comment