Meneja wa klabu ya Everton Ronald
Koeman amesema "amesikitishwa sana" na mashtaka ya kuendesha gari akiwa
mlevi ambayo yanamkabili mchezaji wake Wayne Rooney.
Amesema mchezaji huyo "atachukuliwa hatua" kwa kufuata utaratibu wa klabu.Rooney alikamatwa muda mfupi baada ya saa nne usiku saa za Uingereza usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya polisi wa Cheshire kusimamisha gari lake aina ya VW Beetle eneo la Wilmslow.
Nahodha huyo wa zamani wa England aliachiliwa huru kwa dhamana ana anatarajiwa kufika katika mahakama ya hakimu ya Stockport baadaye mwezi huu.
Mchezjai huyo wa miaka 31 alistaafu soka ya kimataifa Agosti, na bado ndiye mfungaji mabao mengi zaidi katika historia England.
Kikao cha kusikizwa kwa kesi yake kimepangiwa kufanyika tarehe 18 Septemba siku moja baada ya Everton kusafiri kukabiliana na Manchester United mechi ya Ligi ya Premia.
Mechi hiyo itakuwa ya kwanza wka Rooney kurejea Old Trafford tangu aliporejea katika klabu yake ya utotoni, ambayo alikuwa ameihama na kujiunga na United mwaka 2002.
"Tulizungumza Jumanne na mwenyekiti Bill Kenwright amezungumza naye kuhusu hali yake," Koeman amesema.
"Atachukuliwa hatua kwa kufuata utaratibu wa klabu wakati ufaao."
Rooney amefunga mabao mawili na kusaidia ufungaji wa bao moja mechi saba alizochezea Everton msimu huu.
Uchezaji wake umemfanya meneja wa England Gareth Southgate kumtengea nafasi kikosi chake kitakachocheza dhidi ya Malta na Slovakia.
0 comments:
Post a Comment