Wednesday, September 6, 2017

Saa 3 zilizopita Mo Salah alifungia Misri bao pekee mechi hiyo dakika ya sita

Misri walilipiza kisasi kichapo cha Ijumaa mikononi mwa Uganda mjini Kampala kwa kuwalaza 1-0 mjini Alexandria na kuongoza tena Kundi E Jumanne.
Mohamed Salah alifunga bao la ushindi dakika ya sita, jaribio lake la pili baada ya kipa wa Uganda Dennis Onyango kuzuia kombora lake la kwanza kuingia.
Onyango alifanya kazi ya ziada kuzuia Uganda kushindwa.
Kulikuwa na sherehe kubwa mwisho wa mechi hiyo miongoni mwa raia wa Misri, ambao hawajashiriki Kombe la Dunia tangu 1990 licha ya kushinda mataji manne ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika tangu wakati huo.
Misri sasa wana alama tisa, Uganda saba nao Ghana - ambao walicheza fainali tatu zilizopita za Kombe la Dunia - wakiwa nafasi ya tatu na alama tano baada ya kulaza Jamhuri ya Congo 5-1 mjiniBrazzaville.
Congo, wana alama moja pekee, na hawawezi tena kufuzu kwa michuano hiyo itakayofanyika Urusi mwaka ujao

0 comments:

Post a Comment