Winga wa zamani wa Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara,Simon Msuva kwa mara ya
kwanza ataichezea timu ya Mpya kwenye Ligi Kuu ya Morocco,Maarufu kama
‘Botola’
Pazia La Ligi Kuu ya Morocco
lilifunguliwa jana kwa mechi mbili zilichezwa hivyo Msuva na timu yake
ya Difaa El Jadid watashuka kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Ben Ahmed
El Abdi Mjini El Jadida kucheza na Chabab Atlas Khenifra.
Msuva ambaye ni Mfungaji bora wa
Ligi Kuu ya Tanzania msimu wa 2017-18 alijiunga na Wamorocco hao
akitokea klabu ya Yanga na tayari amecheza mechi 11 akiwa na Difaa El
Jadida huku akiwa amefunga jumla ya magoli 9 kwenye mechi za Majaribio
hivyo tunaimani atauwasha moto kwenye Ligi hiyo ngumu.
0 comments:
Post a Comment