Sunday, September 10, 2017


Rafael Nadal
Nyota namba moja kwa ubora kwa upande wa wanaume Rafael Nadal atacheza fainali ya michuano ya Us Open dhidi ya Kevin Anderson.Nadal alimuondosha Juan Martin del Potro kwa seti tatu kwa ushindi wa 6-0 6-3 6-2 katika mchezo wa nusu fainali.
Anderson raia wa Afrika Kusini mwenye miaka 31 alimuondosha Pablo Carreno Busta kwa 7-5 6-3 6-4
Akiwa nambari 32 duniani, Anderson ni mchezaji aliyeorodheshwa wa chini zaidi kufika hatua hiyo ya fainali huko Flushing Meadows yangu kuanzishwa kwa mfumo huo wa uorodheshaji mnamo 1973.
Anakabiliwa na changamoto kubwa dhidi ya Nadal, aliye na rekodi ya 4-0 na rekodi hiyo imezidi uzito katika mpambano dhidi ya Del Potro aliyeonekana kuchoka.
"Ina maana kubwa," amesema Nadal. "Umekuwa msimu mzuri kwa hakika, baada ya kupata matatizo kiasi na majeraha pia".
Nadal atakuwa akiwania Grand slam yake ya kumi na sita na taji lake la tatu la US Open, Mchezo wa fainali utapigwa kesho

0 comments:

Post a Comment