9 Septemba 2017
Ligi ya England inaendelea tena leo saa kumi na moja jioni kwa saa za Afrika mashariki itacheza michezo mitano ya ligi hiyo.
Washika
mitutu wa London Arsenal watakuwa nyumbani katika dimba la Emirate
kuwalika Afc Bournemouth, wageni wa ligi Brighton & Hove Albion wao
watakuwa wenyeji wa West Bromwich Albion.Arsenal haina wasiwasi kuhusu afya ya wachezaji wake, mchezaji pekee aliyejeruhiwa Santi Cazorla - hayupo katika kikosi cha wachezaji 25.
Jack Wilshere huedna asiweko kutokana na ukosefu wa mazoezi ya mechi, lakini Alexandre Lacazette na Sead Kolasinac wanatarajiwa kuitwa kushiriki.
Kapteni wa Bournemouth Simon Francis yupo fiti baada ya kukosa mechi mbili zilizopita za ligi kutokana na jeraha la msuli wa hamstring.
Everton wao watakuwa wenyeji wa Tottenham Hotspurs, bingwa mtetezi Chelsea atakua ugenini katika dimba la King Power kukipiga na Leicester City.
Watakatifu wa Southampton watakua nyumbani St Marrys kukipiga na Watford na mchezo wa mwisho utawakutanisha Stoke City watawakaribisha Mashetani wekundu wa Man United.
0 comments:
Post a Comment