Sunday, September 10, 2017

Na Thomas Ng’itu
Kocha msaidizi wa Klabu ya Simba Jackson Mayanja amesema licha ya kuwa klabu yake kutopoteza katika michezo yake ya kirafiki na ligi bado wana utata katika nafasi ya umaliziaji.
Mayanja amesema mabeki, viungo na washambuliaji wote wazuri, lakini bado kuna tatizo katika safu yao ya ushambuliaji, katika umaliziaji.
“Hatupotezi kweli kwasababu mabeki wanazuia na hata viungo wanatengeneza nafasi, lakini katika ushambuliaji bado tunataka tufanyie kazi ili kutumia nafasi ambazo zinakuwa zinatengenezwa na hazitumiwi vizuri,” Mayanja.
Akizungumzia kuhusu suala la uwanja wa Azam Complex, amesema kama CAF wameruhusu uwanja uchezewe mechi za kimataifa, basi ni uwanja ambao vigezo vimekidhi kutumika.
Wakati huo huo kocha Mkuu wa Azam Aristica Cioaba amesema walistahili kupata ushindi katika mchezo huo, lakini hali ilibadilika.
“Simba ina wachezaji wazuri kama Aishi, Nyoni, ambao tulikuwa nao hapa awali, ni wachezaji wazuri, tulitaka kutoka na ushindi lakini matokeo ndio yametoka hivi,” Cioaba.

0 comments:

Post a Comment