Saturday, September 9, 2017

8 Septemba 2017 . Arsenal walikaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21.

Arsenal wana imani kwamba wataweza kufufua makubaliano ya kulipa £92m kumchukua kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Thomas Lemar, 21, dirisha ndogo la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa Januari. (Star)
Gunners pia wanataka kumnunua mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller, 27, lakini Chelsea, Liverpool na Juventus wote pia wanammezea mate mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani (Tuttosport, kupitia Talksport)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anatarajiwa kufanya mazungumzo na klabu hiyo mwezi Novemba kuhusu kurefusha mkataba wake. (Telegraph)
Kiugno wa kati wa Slovakia ambaye amekuwa akitafutwa na Manchester United Marek Hamsik, 30, amekiri kwamba itakuwa vigumu sana kukataa ofa kutoka kwa mashetani hao wekundu. (Mirror)
West Ham wanapanga kuwasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno William Carvalho, 25, mwzi Januari licha ya kwamba walishindwa kumnunua majira ya sasa ya joto. (Sun)
Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amesema anasalia na matumaini kwamba mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania Diego Costa, 28, atarejea katika klabu hiyo Januari. (Marca)
Lille waliikataa nafasi ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Vincent Janssen, 23, kwa sababu mkufunzi wao mkuu Marcelo Bielsa alikuwa na shaka kuhusu uwezo wa kiufundi wa mshambuliaji huyo wa Tottenham. (SFR Sport, kupitia London Evening Standard)
Valencia walipanga kumchukua kwa mkopo kiungo wa kati wa Tottenham Moussa Sissoko, 28, majira ya joto lakini baadaye waliamua kumchukua mchezaji wa Manchester United wa miaka 21 Andreas Pereira. (Super Deporte, kupitia Talksport)
William Carvalho
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption William Carvalho alichezea timu ya taifa ya Ureno mara ya kwanza 20132016
Fowadi wa Paris St-Germain Julian Draxler amewaambia wenzake timu ya taifa ya Ujerumani kwamba alitaka kuhamia Barcelona majira ya joto. Mchezaji huyu wa miaka 23 alikuwa amehusishwa na kuhamia Arsenal. (Mundo Deportivo, kupitia Metro)
Kiungo wa kati wa Napoli Marek Hamsik, 30, amesema fursa ya kuhamia Manchester United inaweza kumpa kibarua cha kufanya uamuzi mgumu zaidi maisha yake ya uchezaji. (Kicker, kupitia Star)
Kiungo wa kati mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, hatarejeshwa moja kwa moja kikosini kwa sababu meneja Jurgen Klopp anaamini mchezaji huyo wa Brazil hayuko sawa tayari kucheza. (Mail)
  Ahmed Musa
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Musa alijiunga na CSKA Moscow mwaka 2012 na kufunga mabao 54 mechi 168
Barcelona wanamtaka mshambuliaji wa Ufaransa anayechezea Marseille Maxime Lopez, 19. (Mundo Deportivo )
Hull City walikuwa walikaribia kumchukua mshambuliaji wa Leicester City Ahmed Musa, 24, kwa mkopo siku ya mwisho ya kuhama wachezaji. (Hull Daily Mail)
Derby County nao wanawatafuta wachezaji ambao hawana mikataba baada ya kushindwa kumnunua kiungo wa kati Mholanzi Maikel Kieftenbeld wa miaka 27 kutoka Birmingham. (Derby Telegraph)
Nahodha wa Celtic Scott Brown, 32, naye bado hajaafikiana kuhusu mkataba mpya na mabingwa hao wa ligi ya Scotland. (Daily Record)

0 comments:

Post a Comment