8 Septemba 2017
Meneja wa
Manchester Pep Guardiola amesema hakukuwa na uwezekano wowote kwamba
Manchester City wangemuongeza Raheem Sterling kwenye mkataba wa kumnunua
mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez.
Arsenal walikuwa
wameafikiana na City uhamisho wa £60m kwa Sanchez, 28, lakini hilo
lilitegemea kufanikiwa kwa Gunners kumchukua Thomas Lemar.Lemar hata hivyo aliamua kusalia Monaco.
Guardiola amesema Gunners walitaka Sterling, 22, kama sehemu ya mkataba wa kumuuza Sanchez.
- Sababu ya Alexis Sanchez kukosa kuondoka Arsenal
- Klabu za England zilivyovunja rekodi kuwanunua wachezaji
- Man City yailaza Bournemouth, Sterling apewa kadi nyekundu
"Tulisema tulitaka kuwalipa pesa taslimu kwa ajili ya Alexis. Walikubali lakini hawangeweza kumnunua mchezaji waliyemtaka, kwa hivyo alisalia Arsenal."
Sterling amechezea City mechi tatu msimu huu na kufunga mabao mawili.
Alifukuzwa uwanjani kwa kusherehekea sana bao la dakika za mwisho la ushindi dhidi ya Bournemouth kabla ya mapumziko ya kimataifa.
Alichezea England mechi mbili wakati wa mapumziko ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment