Friday, September 8, 2017


        P 1
KAMATI ya Utendaji ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), iliyokutana Dar es Salaam jana Septemba 7, 2017, imepanga Uchaguzi Mkuu wa chama hicho ufanyike Novemba 5, mwaka huu.
Uchaguzi huo utafanyika Dar es Salaam katika ukumbi ambao utatangazwa na tayari kamati imeaigiza sekreterieti ya TASWA, ifanye maandalizi kuhusu uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ajili ya usimamizi wa karibu.
Kikao kimekubaliana watakaoshiriki uchaguzi huo ni wanachama wote wa TASWA waliopo katika leja kuanzia Juni mwaka 2007 hadi Juni mwaka 2017, wakiwemo walioingia uanachama wakati wa semina ya waandishi chipukizi iliyofanyika Dar es Salaam Agosti mwaka 2015 na sharti kubwa ni kila mwanachama kulipia ada ya mwaka mmoja.
Kwa wanachama wengine wapya wanaotaka kujiunga, watafanya hivyo baada ya uongozi mpya kuingia madarakani na kupewa utaratibu kulingana na Katiba ya chama inavyoeleza na pia kwa kadri uongozi mpya utakaoingia madarakani utakavyoona inafaa.
Kutokana na hali hiyo wanachama wote wenye sifa hizo, wanatakiwa kulipia ada zao kwa Mhazini Msaidizi, Zena Chande kuanzia leo hadi Septemba 30, mwaka huu.

Uongozi wa sasa wa TASWA uliingia madarakani mwaka 2014, ambapo Juma Pinto alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Egbert Mkoko (Makamu Mwenyekiti), Amir Mhando (Katibu Mkuu), Grace Hoka (Katibu Mkuu Msaidizi), Shija Richard (Mhazini) na Zena Chande (Mhazini Msaidizi).

Wajumbe ni Rehure Nyaulawa, Chacha Maginga, Mussa Juma, Mwani Nyangassa, Mroki Mroki, Ibrahim Bakari na Majuto Omary anayeingia kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa TASWA FC.

Ahsanteni,

Juma Pinto
Mwenyekiti TASWA
08/09/2017

0 comments:

Post a Comment