Borussia Dortmund watakopoumana na
Freiburg kwenye Bundesliga, matokeo tayari yameshafahamika na wengi,
kwani michezo 12 ambayo timu hizo zimekutana maokeo yalikuwa dhahiri.
Dortmund watasafiri kuelekea dimba la Schwarzwald Stadion mjini Freiburg
wakiwa wameshinda mara 12 dhidi ya timu hiyo, huku Freiburg mara ya
mwisho wakishinda mwaka 2010.
Na kama haitoshi, Dortmund kiwango
Bora kabisa na inaashiria ushindi tayari ni halali kwao. Dortmund wako
kwenye kilele cha Msimamo wa ligi ya Bundesliga wakiwa wamejikusanyia
point 6 kutoka katika michezo miwili ambayo wameshacheza huku Freiburg
wakiwa na pointi moja tu baada ya kutoka sare na Frankfurt.
Kitu kinachoweza kuwapa hamasa
Freiburg ni kwamba wachezaji wengi wa Dortmund wametoka kutumikia timu
zao za Taifa hivyo watakibiliwa na uchovu tofauti na ilivyo kwa
wachezaji wa Freiburg ambao waliendelea na mazoezi. Pia kuondoka kwa
mfaransa Ousmane Dembele pengine kutawapunguzia kasi Dortmund.
Kwa upande mwingine Maximilian
Philipp ambaye amenufaika na kuondoka kwa Dembele, msimu ulipoita
alikuwa kipenzi cha Mashabiki katika dimba la Schwarzwald Stadion. Maxi
alitimkia Dortmund kwa ada ya uhamisho ya Pauni mil. 20 na sasa
amejihakikishia namba katika kikosi cha Kwanza cha Borussia Dortmund
baada ya Dembele kuondoka klabuni hapo. Maximilian Philipp sasa anacheza
pamoja na Mgabon tishio Pierre Emerick Aubameyang.
Mturuki Nuri Sahin aliyejiunga
na Real Madrid mwaka 2011 akitokea Dortmund kabla ya kurejea tena
akipitia Liverpool, anasema anaelewa kwa nini Dembele ametimkia
Barcelona.
“Sisi sio Barcelona na
tumezungumza kwamba kama Barcelona wanaweza kumpoteza Neymar, sisi
hatuwezi kujificha, kwenye ulimwengu wa Soka siku zote kuna hatua ya
zaidi yako, sisi pia tunanunua wachezaji kutoka klabu nyingine, hii
itaendelea kuwepo”
Jumamosi hii watazamaji kote
Africa wataweza kutazama LIVE mchezo kati ya Freiburg na Borussia
Dortmund utakaorushwa MUBASHARA kupitia StarTimes ambao wana kibali
Pekee cha kuonyesha matangazo hayo.
0 comments:
Post a Comment