Friday, September 8, 2017


FB_IMG_1494602000921
Mchezo  namba 10 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC dhidi ya Simba, sasa utafanyika saa 10.00 jioni badala ya muda awali uliopangwa wa saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limebadilisha muda huo kutokana na kuagizwa na Jeshi la Polisi kuipeleka mechi hiyo jioni kutokana na sababu za kiusalama, ikidai ni hatari kufanyika usiku.
Kikosi cha Azam FC kinatarajia kumalizia maandalizi ya mwisho leo Ijumaa jioni kuelekea mchezo huo, ambao utachezeshwa na mwamuzi Ludovick Charles wa Tabora, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Abdallah Mkomwa wa Pwani.
Mwamuzi wa mezani atakuwa Josephat Bulali huku Kamisaa atakuwa Ruvu Kiwanga, wote wa Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment