Baada ya timu ya taifa ya Italia kushindwa kufuzu kwa fainali za michuano ya kombe la dunia litalofanyika nchini Italia mwakani, nyota wanne wa timu hiyo wameamua kubwaga manyanga.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Italia kukosa michuano hiyo tangu 1958, tangu baada ya kukosa michuano hiyo Italia walifuzu kwa fainali hizo mara 14 mfululizo ikiwa ni idadi ya 3 kwa ukubwa kufuzu mfululizo.
Buffon ambaye baada ya mchezo alionekana kutokwa na machozi amesema anajisikia vibaya sana na aibu kwa jinsi ambavyo anaachana na timu ya taifa huku wakiwa wameshindwa kuipeleka kombe la dunia.
Buffon ameichezea timu ya taifa michezo 172 katika miaka 20 ndani ya timu hiyo huku katika michezo hiyo amefanikiwa kupata clean sheets 77 katika timu ya taifa.
Naye mlinzi wa klabu ya Juventus Giorgio Chiellini bado hajatoa taarifa kamili kuhusu kuachana na timu hiyo ama laa lakini inaaminika naye anaona ni muda sasa umefika kuondoka.
Andrea Barzagli naye amekiri kwamba ni aibu kubwa sana kwa timu yao kushindwa kushiriki kombe la dunia na hadi sasa haamini kile kilichotokea lakini hivyo ndivyo imetokea.
Hili ni pigo kubwa kwa Waitaliano kwani wachezaji wote wanne walikuwepo katika kikosi kilichoipa Italia kombe la dunia 2002 na kwenda fainali Euro 2012 na sasa unaweza kuwa muda wa kizazi kipya nchini Italia.
0 comments:
Post a Comment