Watford imekataa ombi kutoka kwa Everton kwa meneja wao raia wa Ureno wa kiwango cha juu Marco Silva.
Silva,
40, amekuwa nahodha kwa michezo 11 ya Ligi ya Premia katika uwanja wa
Watford wa Vicarage Road baada ya kuiaga Hull City kufuatia kushushwa
daraja msimu ujao. Everton ilikuwa inamatamanio ya kumteua Silva baada ya kumpiga kalamu meneja wake Ronald Koeman , lakini Hornets wako tayari kumpinga mtu yeyote atakayejaribu kumrai Silva kuiga klabu hiyo.
Kilichosalia nikuona iwapo Toffees itazidisha matamanio yao kwa kocha huyo.
Kocha wa Everton ,23, David Unsworth kwa hivi sasa anashikilia nafasi ya umeneja baada ya Koeman kupigwa kalamu chini ya saa 24 baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-2 kutoka kwa Arsenal tarehe oktoba 22.
Unsworth ameshinda mechi moja pekee kati ya nne ambazo amekuwa akiongoza, ushindi ambao umekejeliwa wa mabao 3-2 baada ya kutoka nyuma na kupata magoli mawili.
Meneja wa zamani wa Englang Sam Allardyce amehusishwa na Everton kuweza kuiongoza klabu hiyo kwa kipindi cha muda mfupi, huku meneja wa Burnley Sean Dyche ni jina lengine lilitajwa kuigoza katika uwanja wa Liverpool Goodison Park.
0 comments:
Post a Comment