Thursday, December 14, 2017


 Furry ni miongoni mwa mabondia wa Uingereza waliotamba mwaka 2015

Bondia wa uzito wa juu wa Uingereza Tyson Fury ametaka kupewa pambano la haraka baada ya kurejea tena katika ndondi.
Fury aliyefungiwa kushiriki mchezo huo mwaka 2016 kwa sababu sampuli zake zilisemekana kuonyesha kutumia dawa za kusisimua misuli, ametaka pia kurudishiwa mikanda yake mara moja.
Bondia huyo mwenye miaka 29 tiyari ameonyesha nia ya kupambana na mkali wa uzito wa juu Anthony Joshua mwaka 2018.
Promota wa Joshua, Eddie Hearn amesema ni jambo jema na anaamini Furry atachapwa ndani ya raundi tano.
Furry alipatikana na hatia ya kutumia dawa zilizokataliwa michezoni na kwa sasa adhabu yake inafikia ukingoni.

0 comments:

Post a Comment