Thursday, December 14, 2017

Rekodi mpya imewekwa na Manchester City hii leo ya kushinda michezo 15 mfululizo wakiipiku rekodi ya Arsenal ambao walishinda michezo 14 mfululizo, Man City waliibuka leo kidedea kwa kuichapa Swansea mabao 4 kwa sifuri.
Wayne Rooney aliwafungia bao pekee Everton wakati wakiiua Newcastle bao 1 kwa 0, na sasa Wayne anakuwa ameifunga Newcastle mabao 15 katika EPL idadi ambayo ni kubwa kuliko aliyowahi kuifunga timu yoyote.
Romelu Lukaku aliifungia Manchester United bao pekee ambalo linamfanya kuzifunga mabao 30 kati ya mechi 38 timu ambazo hazikuwa top six msimu uliopita kuanzia mwanzo mwa msimu wa 2016/2017.
Arsenal walikwenda suluhu bila kufungana na West Ham huku Liverpool nao wakitoka sare ya bila kufungana zidi ya West Bromich Albion na Tottenham Hotspur wakiwa nyumbani waliichapa Brighton bao 2 kwa nunge.
Matokeo ya hii leo yamewapeleka Arsenal hadi nafasi ya saba huku Tottenham Hotspur wakipanda hadi nafasi ya nne ya msimamo wa PL ambao Manchester City ndio viongozi wa ligi hiyo.

0 comments:

Post a Comment