Arsene Wenger awapiga bao Mourinho na Conte kwa kiungo huyu
Chelsea na Manchester United wameripotiwa kwa nyakati tofauti kutafuta saini ya kiungo wa zamani wa klabu ya Stoke City ambaye kwa sasa anakipigia katika klabu ya Sevilla Steven Nzonzi.
Nzonzi msimu huu amekuwa katika kiwango cha juu sana kiasi cha kuvifanya vilabu vingi kutamani saini yake lakini sasa taarifa zinasema kiungo huyo ameshafanya makubaliano na Arsenal tayari kwa kujiunga nao January.
Nzonzi ana mkataba na klabu ya Sevilla lakini katika mkataba huo kulikuwa na kipengele ambacho Sevilla wangeweza kumuuza Nzonzi kama kuna timu itakuwa tayari kutoa ada ya kiasi cha £35.2m.
Jarida maarufu la michezo nchini Hispania la El Gol limetoa ripoti inayosema tayari kila kitu kinaonekana kwenda sawa kati ya Nzonzi na Arsenal ambapo katika dirisha la usajili la January anaweza kuvaa jezi ya Gunners.
Usajili wa Nzonzi unaweza kuwa msaada mkubwa kwa Arsenal ambapo wanaonekana kuhangaika sana katika nafasi ya kiungo ambayo kwa misimu kadhaa sasa imeonekana kutokaa sawa.
0 comments:
Post a Comment