Thursday, December 14, 2017

Oscar Pistorius (kushoto) akielekea mahakamani mwaka 2016


Mwanariadha wa zamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ameumizwa mkono wake wakati akipigana gerezani wiki chache baada ya kesi ya kumuua aliyekuwa mchumba wake Reeva Steenkamp kusikilizwa tena.
Mwanariadha huyo mlemavu alihusika kati ugomvi wa kugombea simu ya umma, msemaji wa gereza hilo ameiambia BBC.
Pistorius aliyefungwa miaka 13 alikwaruzika ngozi ya mkono kutokana na fujo hizo.
Pistorius alimpiga risasi mchumba wake Reeva Steenkamp siku ya wapendanao mwaka 2013
Hakuna majeraha mengine yaliyotajwa kumpata mwanariadha huyo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Novemba 7, siku kumi baada ya waendesha mashitaka wa Afrika Kusini kukubali adhabu ya kifungo cha miaka sita kilichokuwa kikimkabili Pistorius kuongezwa na kuwa miaka 13.

0 comments:

Post a Comment