RATIBA
ya raundi ya tatu ya Kombe la FA imetoka na gumzo kubwa ni mechi ya
mahasimu wa Merseyside baina ya Liverpool na Everton.
Arsenal
watamenyana na Nottingham Forrest wakati kocha Mreno, Jose Mourinho wa
Manchester United atawakaribisha Derby County Uwanja wa Old
Trafford, Tottenham Hotspur na AFC Wimbledon, Manchester City na Burnley
na Norwich City dhidi ya Chelsea.
Wapinzani
wa The Stanley Park watakutana Uwanja wa Anfield Jumapili kwenye mchezo
wa Ligi Kuu ya England ambao watakutana tena wikiendi ya kwanza ya
Januari.
Mara ya mwisho walipangwa katika hatua hii mwaka 1932 na Liverpool ikashinda 2-1 Uwanja wa Goodison Park.
Hivi
karibuni walikutana kwenye Nusu Fainali mwaka 2012 wakati mabao ya
kipindi cha pili ya Luis Suarez na Andy Carroll yalipoipa Liverpool
ushindi wa 2-1 wakitoka nyuma kwa bao 1-0 la Nikica Jelavic.Ratiba ya raundi ya tatu ya Kombe la FA imetoka na kubwa ni mechi ya mahasimu wa Merseyside baina ya Liverpool na Everton PICHA ZAIDI GONGA HAPA
RATIBA RAUNDI YA TATU KOMBE LA FA ENGLAND
0 comments:
Post a Comment