Tuesday, December 5, 2017


Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2008 kuwaona Real Madrid wakiwa na matokeo yasiyoridhisha katika ligi kuu nchini Hispania kiasi hiki, hadi sasa tayari kidogo kidogo wameanza kupungua katika orodha ya wanaogombania ubingwa La Liga 2017/2018.
Eneo la ushambuliaji la Real Madrid limekuwa butu sana safari hii, msimu wa 2006/2007 ilikuwa msimu wa mwisho kwa Los Blancos kufunga mabao 25 katika michezo 14 kama ilivyo sasa.
Cristiano Ronaldo amepwaya, mashuti 68 aliyopiga yamempa mabao mawili na utatu wao wa BBC umekufa kwani hakuna “connection” yoyote iliyoleta bao kati ya Cristiano Ronaldo na Benzema huku Gareth Bale akiwa ni majeruhi.
Msimu uliopita walikuwa na faida ya suber sub Alvaro Morata ambaye aliwafungia mabao 20 akitokea benchi huku James Rodriguez naye alionekana kuibadili timu kila akiingia lakini kwa sasa wote wawili hawapo.
Tatizo lingine kwa Real linaonekana hawana kiongozi sahihi, Sergio Ramos anashikilia rekodi ya kadi nyekundu nyingi (19) na anaigharimu timu kwani hatakuwepo wakati Real Madrid wakiivaa Sevilla, mchezo ambao unaweza ukaishusha Madrid zaidi au kuipandisha.
Wakala wa Sergio Ramos amedai kwamba siyo kwamba Ramos hana nidhamu bali ni kwa sababu amecheza michezo mingi(416) ndio sababu ya kuwa na kadi nyingi, lakini yupo mtu kama Paulo Maldini mechi 886 kadi nyekundu 4 au Carles Puyol mechi 593 nyekundu 3.
Bado siku zisizozidi 20 kwa pambano la El Classico na Zidane na vijana wake watakuwa katika presha kubwa sana kwani mchezo huu unaweza ukaongeza pengo la alama hadi kufikia 11 tena au wazipunguze hadi kufikia 5.
Dirisha la usajili linakuja na inaonekana ikawa mwokozi pekee wa Real Madrid huku tayari raisi wa klabu hiyo Florentino Perez ameshaonesha nia ya kutaka kufanya usajili mkubwa huku Mo Salah na Neymar wakiwa kwenye orodha ya usajili.

0 comments:

Post a Comment