Tuesday, December 5, 2017

Senagal
Waziri wa michezo wa Senegal, Matar Ba, amesema timu ya taifa ya nchi hiyo itafanya vizuri zaidi katika michuano ya kombe la dunia zaidi ya taifa lolote la Afrika, kwa kufika nusu fainali ya michuano hiyo michuano itayofanyika nchini Urusi mwakani.
Mwaka 2002 kwa mara ya kwanza Senegal iliposhiriki michuano hiyo ilifanya vyema kwa kufika hatua ya robo fainali, Simba wa Teranga wamepangwa katika kundi H, na wakiwa na timu za Poland, Colombia pamoja na Japan.
"Tunapaswa kuwa na malengo yetu - malengo hayo ni kufikia nusu fainali na kufanya vizuri kuliko mwaka wa 2002," Waziri huyo aliiambia BBC.
Waziri Ba akasisitiza kwa kusema "Tuna timu nzuri na bora na tuna kocha wetu raia wa Senegal na tutajitayarisha vizuri kwa ajili ya kwenda kufanya vizuri.
Mchezo wa kwanza wa Senegal watacheza na Poland, June 19 kisha watacheza na Japan tarehe 24, na watamaliza kazi kwa mchezo wa tatu kwa kukipiga na Colombia

0 comments:

Post a Comment