Thursday, January 11, 2018



Ni miezi kadhaa imepita toka Afrika ipokee kwa masikitiko taarifa za kifo cha kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast aliyekuwa anaichezea club ya Beijing Enterprises ya China Cheick Tiote aliyefariki akiwa anafanya mazoezi na timu yake Beijing.
January 10 2018 zimeripotiwa tena taarifa za kusikitisha kuhusu mchezaji Ntaku Zibakaka mwenye umri wa miaka 23 raia wa Congo DRC kufariki mazoezini akiwa na timu yake ya Sagrada Esperança ya Angola kama Tiote.

Ntaku Zibakaka amefariki akiwa yupo  Benguela walipokuwa wameweka kambi na timu yake ya Esparanca kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na alijiunga na vilabu vya Angola 2015 akitokea kwao Congo DRC.

0 comments:

Post a Comment