Mkufunzi wa Chelsea
Antonio Conte ameunga mkono utumizi wa mfumo wa video unaowasaidia
marefa baada ya timu yake kutoka sare tasa na Arsenal katika nusu
fainali ya kombe la Carabao mkondo wa kwanza.
Refa Martin Atkinson
alitumia mfumo huo wa VAR kwa madai mawili ya penalti ya Chelsea wakati
ambapo Victor Moses aligongana na Maitland-Niles katika kipindi cha
kwanza na wakati Danny Welbeck alipomkabili Cesc Fabregas , na alifurahi
kwamba ushahidi alioonyeshwa haukuwa wa kutoa panalti.''Nafurahia utumizi wa VAR kwa sababu kunapokuwa na wasiwasi wakati wa mechi ni vyema wakati refa na wasaidizi wake wanapoangalia video hiyo na kutoa uamuzi mwafaka'', alisema Conte.
''Nadhani kila mtu anataka makosa machache wakati wa mechi na nadhani hilo litasaidia sana''.
Timu hizo mbili zitakutana tena katika mkondo wa pili katika uwanja wa Emirates mnamo tarehe 24 mwezi Juni baada ya Arsenal kuonyesha ukakamavu kufuatia kushindwa kwao katika kombe la FA na klabu ya Nottingham Forest.
''Arsenal ilicheza vizuri'', alisema Wenger.
''Tulikuwa tumejiandaa na ilikuwa sare nzuri na sasa ni lazima kumaliza kazi tulioanza''.
0 comments:
Post a Comment