Sunday, January 7, 2018


Mbrazil Philippe Coutinho amesaini mkataba wa miaka mitano na nusu kujiunga na Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


Takwimu za Coutinho Liverpool 

2012-13 Mechi 13, mabao 3
2013-14 Mechi 37, mabao 5
2014-15 Mechi 52, mabao 8
2015-16 Mechi 43, mabao 12
2016-17 Mechi 36, mabao 14
2017-18 Mechi 18, mabao 12 
HATIMAYE Philippe Coutinho ni mchezaji mpya wa Barcelona ya Hispania baada ya uhamisho wa Pauni Milioni 145 kutoka Liverpool.  
Picha zilimuonyesha kiungo huyo Mbrazil akisafiri kwenda Hispania kupitia London jana jioni na baadaye Barca ikatangaza rasmi kukamilisha uhamisho wake. 
Coutinho, mwenye umri wa miaka 26 thamani yake baada ya kutua Barcelona ni Pauni Milioni 355 katika mkataba wa miaka mitano na nusu aliosaini.
Coutinho anatarajiwa kuishuhiudia Barcelona katika mchezo wa nyumbani wa La Liga na Levante mchana wa leo. 
Kwa uhamisho huu, Coutinho anakuwa mchezaji wa pili ghali kihistoria duniani, baada ya Mbrazil mwenzake, Neymar, aliyeondoka Barcelona kujiunga na Paris Saint-Germain kwa Pauni Milioni 198 mwanzoni mwa msimu. 

0 comments:

Post a Comment