Inaonekana kama Sergio Kun Aguero amekuwa akiinoea zaidi Newcastle kwani baada ya ile hattrick yake dhidi ya timu hiyo mwaka 2015 hii leo tena Kun Aguero amewafunga Newcastle hattrick nyingine.
Baada ya mabao yake matatu ya leo sasa Aguero anakuwa ameifunga Newcastle jumla ya mabao 13 na ni Wayne Rooney (15) pekee mwenye mabao mengi kuliko Aguero katika ligi kuu ya EPL.
Lakini wakati Aguero akiongeza namba yake ya magoli, Kelvin De Bruyne naye amefikisha hattrick 10 na sasa anakuwa mchezaji mwenye assist nyingi zaidi katika EPL akimzidi Paul Pogba mwenye 9.
Wakati Manchester City wakifanya hivyo, wapinzani wao Manchester United waliwafunga bao 1 kwa nunge Burnley na sasa David De Gea anakuwa golikipa mwenye clean sheets nyingi (14) katika ligi kuu 5 barani Ulaya.
Alexandre Lacazette alifunga moja ya bao wakati Arsenal wakiifunga Crystal Palace bao 4 kwa 1 lakini bao la Lacazette lilikuwa bao la 400 kwa klabu ya Arsenal kutoka kwa wachezaji wazawa wa Ufaransa.
Lakini pia mabao 3 waliyofunga Arsenal katika dakika 13 za mwanzo ndio mabao mengi yaliyofungwa kwa muda mfupi zaidi tangu Arsenal wafanye hivyo dhidi ya Newcastle February mwaka 2011.
Mabao 2 ya Eden Hazard yamemfanya kukaa juu ya Ginfranco Zola katika kuhusika na mabao ndani ya klabu ya Chelsea ambapo sasa Mbelgiji huyo anakuwa amefunga mabao 65 na kuassist mabao 37 ndani ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment