Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa Kamati ya
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Duniani (FIFA) (hawapo pichani) unaotarajia kufanyika nchini mwezi
Februari 2018 kuhakikisha maandalizi yanakuwa mazuri ili ujio huo
uwezekuletea manufaa kwa taifa katika kikao kilichofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi
ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani
(FIFA) wakisililiza maagizo ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliyokuwa akitoa katika kikao hicho kwa
lengo la kufanikisha ujio huo wa Kimataifa kuwa unaleta manufaa kwa
taifa jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Duniani (FIFA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe katika kikao
cha maandalizi ya ujio huo kilichofanyika jana jijini Dar es
Salaam,wapili kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo
kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Yusuph Singo.
0 comments:
Post a Comment