Sunday, January 21, 2018

KONGO imekata tiketi ya Robo Fainali ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso jana Uwanja wa Agadir, Morocco.
Mabao ya Kongo jana yalifungwa na nyota wake tegemeo, Carof Bakoua dakika ya 67 na Kader Bidimbou dakika ya 90.
Kwa ushindi huo, Kongo inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili, ikifuatiwa na Angola pointi nne na Burkina Faso pointi moja, wakati Cameroon haina ponti.
Michuano hiyo itaendeleaa leo kwa mechi za kukamilisha mzunguko wa tatu wa hatua ya makundi, wenyeji Morocco wakimenyana na Sudan na Mauritania wakimenyana na Guinea, mechi zote zikianza Saa 4:00 usiku.

0 comments:

Post a Comment