MSHAMBULIAJI
Alexis Sanchez amewasili Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimko vya
afya makao makuu ya klabu viwania vya Carrington leo ili kukamilisha
uhamisho wa kubadilishana wachezaji kutoka Arsenal.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameweka wazi kwa kusema; "Nafikiri tunaelekea kufanikiwa,".
Kiungo
wa United, Henrikh Mkhitaryan amefikia makubaliano ya vipengele binafsi
na Arsenal, lakini pia The Gunners wameanza mazungumzo ya kumununua kwa
Pauni Milioni 44 mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick
Aubameyang.
Ofa yao ya kwanza ilikataliwa, lakini wanatarajiwa kupeleka nyingine.
Hatimaye Manchester United imekamilisha usajili wa Alexis Sanchez kutoka Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Pamoja
na hayo, Mourinho alisema baada ya mechi na Burnley, United wakishinda
1-0 kwamba alijua mwishowe atampata mchezaji huyo.
Sanchez,
mwenye umri wa miaka 29, ataingiza kiasi cha Pauni 450,000 kwa wiki
katika mkataba wa miaka minne na nusu Old Trafford baada ya United
kubomoa benki kuwapiku mahasimu wake, Manchester City na Chelsea.
Leo
Sanchez alitarajiwa kuwasili mapema Carrington kati ya Saa 7:00 mchana
na Saa 9:00 Alasiri wakati wachezaji wenzake wapya wamepewa siku mbili
za mapumziko kuelekea mechi ya Kombe la FA ijumaa dhidi ya Yeovil na
Jose Mourinho amesafiri kwenda London kukaa na familia yake nyumbani.
0 comments:
Post a Comment